Intro ahhh...ahhhh ohhh yeahhh..(shhhh!).. it\'s the remix (shhhh!)...JCB....(ahhhh!).....Murder..! (Tongwe Records Babyyyy) Verse 1 (JCB) Damu ilitapakaa baada ya ule mlio kulia PAAA, Watu wote walisambaa hata walevi wa kwenye bar, Sio polisi sio baunsa iliye kaa utashanga kwa nini mshkaji alizidi kumimina kwa kujiamini, Amini usiamini akabaki tu na mimi, Akanishikia bunduki kwa chini, Akadai eti nimpe madini lasivyo ananipiga risasi kama sabini, Anasura kama idi amini akarudi karibu atua tatu mpaka kabatini, Akatamka HEYOO! nipo kazini nimetumwa mzigo au ujithamini, Akanikanyaga kwa chini kikorofi bunduki tena akaikoki Akasema kama simuonyeshi leo sio koki,jinsi alivyo akilenge ye akosi mikosi, Kavaa koti jeusi jasusi, Mikono nikaweka juu kuepuka nukx huku natukana mengi matusi... Chorus X2 Ukisikia PAAAA...ujue imekukosa Aliyelenga hana shabaha...amefanya makosa Ukisikia PAAAA...ujue imekukosa Aliyelenga hana shabaha...amefanya makosa Verse 2 (Fid Q) Wanasema hugeuka mnyama sana anaposaka pesa Cha ajabu anavuta bangi lakini hawazii magangstar Hampaki rangi donkey ili ageuke kuwa zebra Ndo maana kabla hajaikoki, JCB ali-surrender Akajifanya hayuko na mie ili niipigie defender Nikaona vipi nijistukie ghafla nikasikia \'\'RASTA\'\' Jambazi linaniita halafu sioni wakuni-backup Hali inatisha sikuongea nilishut the fluck up Akaniuliza.. we sio Fid Q yule anayeheshimika mtaani ? Nikamwambia ndo mimi na huu ndo muda wa kumlaani shetani Sie wote ni watoto wa mjini siamini vipi hatujuani Mie alwatani kama Kwere au Chindo popote amani Akaniambia.. waambie machizi i\'m sorry, leo mna-rap wapi ? Mie sio mtu wa stories, i make things happen Hii sanaa ni ya watengwa na ngosha... Ukisikia Paaaaaaaa........ ujue imekukosa Chorus X2 Ukisikia PAAAA...ujue imekukosa Aliyelenga hana shabaha...amefanya makosa Ukisikia PAAAA...ujue imekukosa Aliyelenga hana shabaha...amefanya makosa Verse 3 (Jay Moe) (aahhh!) Alipogundua ni wasanii,haraka haraka akatuacha Ndipo tulipomsihi,na watu wengine kuwaacha Maana ishakuwa msala,na mashahidi nyuzi washavuta So muda wowote defender,toka hivi sasa itafika Bora usepe..kuliko kupewa kesi ya mauaji Au kesi ya kujaribu,kupora kwa kutumia mkwaju Hakuna mwenye mzigo,waambie wenzako mme-boogie Na wala hatuna kimango,usione mezani kinywaji Achana na mambo ya leo,wapi tunapiga show Pigia wenzako simu,waambie huku ni soo Hakuna mtu wa madini,sema ni kina jaymoe Kabla haujaishia mikononi,kwa gorvo..au you know ! Ile anaanza kuchomoka tu,polisi washawasili Nikasikia mikono juu..kwa sauti ya ukali Kukimbia akala ya mguu,akasalimu amri Akanyoosha mikono juu Chorus X2 Ukisikia PAAAA...ujue imekukosa Aliyelenga hana shabaha...amefanya makosa Ukisikia PAAAA...ujue imekukosa Aliyelenga hana shabaha...amefanya makosa Verse 4 (Chidi Benz) Hata police ni mdili na ndo mchongo ameupanga.. Na ndo yeye wamemtuma jukumu lake kuwa mwanga... na ile paaahh!! Kama Suka kama kulenga mchanga Mwisho wa siku mahesabu watu wakacheze fanga Mchezo kamili ulishapangwa yaliyopita ni historia... na maneno kaa ya kwenye kanga ya hesabu nishatulia Wa kucheka wamecheka wa kulia wamelia Nchi bado haikufea so hamtochoka kusikia Michezo kama hii kurudia ninajua walala hoi Wamechoka vumilia...yeeahh Damu zitamwagika kwa wema na wasio wema... na imani ya mkabaji ulichokimeza utakitema Kuna movie ila maisha ka cinema Unyang\'anyi na uchukuzi unaoatokeo kila nikihema ...(hema) Wanasema ukila nyama....lazima utake tena.. na kweli macho kwa maneno ya viongozi wanaosema Ni vigumu kutumkia kabla tonge kuingia So anytime tuwe tayari kuumia....yeeahh Ni vigumu kutumkia kabla tonge kuingia So anytime tuwe tayari kuumia....yeeahh Chorus X2 Ukisikia PAAAA...ujue imekukosa Aliyelenga hana shabaha...amefanya makosa Ukisikia PAAAA...ujue imekukosa Aliyelenga hana shabaha...amefanya makosa
File download Mp3 Full Album kami compres menggunakan rar dan disimpan melalui hosting 4shared.com dan mediafire.com, file rar tidak menggunakan Password. How To Download